Genesis 27:20-24

20Isaka akamuuliza mwanawe. “Umepataje haraka namna hii, mwanangu?”

Akajibu, “Bwana Mwenyezi Mungu wako amenifanikisha.”

21Kisha Isaka akamwambia Yakobo, “Mwanangu tafadhali sogea karibu nami ili nikupapase, nione kama hakika ndiwe Esau mwanangu, au la.”

22Yakobo akasogea karibu na baba yake Isaka, ambaye alimpapasa na kusema, “Sauti ni ya Yakobo, bali mikono ni ya Esau.” 23Hakumtambua, kwa sababu mikono yake ilikuwa na nywele kama ya ndugu yake Esau, kwa hiyo akambariki. 24Akamuuliza, “Hivi kweli wewe ni mwanangu Esau?”

Akajibu, “Mimi ndiye.”

Copyright information for SwhKC